KATIKA kuboresha huduma za afya benki ya NMB imetoa vitanda vitano na mashuka 100 kwenye Hospitali ya Msoga Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Aidha benki hiyo imetoa madawati 120 kwa Shule za Msingi Mwetemo madawati 70 na Misani madawati 50 ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati.
Akipokea misaada hiyo hospitalini hapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete ameishukuru benki hiyo kwa kusaidia sekta hizo za elimu na afya.
Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze amesema kuwa hadi sasa benki hiyo imeshatoa misaada mbalimbali yenye thamani ya shilingi milioni 88 ambapo hata mashuka ya kwanza kwenye Hospitali hiyo yalitolewa na benki hiyo.
Naye Mkuu wa Idara ya Mauzo na Mtandao wa matawi wa Benki ya NMB Donatus Richard Kwa upande wake Donatus Richard ambaye alimwakilisha Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB amesema kuwa wanatenga asilimia moja ya faida kila mwaka kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, afya na majanga.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga amesema kuwa anaishukuru benki hiyo kwa kutoa vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kupitia sekta hizo.
No comments:
Post a Comment