Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo
(kulia), akitoa maelezo kwa mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Raphael Enock, kuhusu
elimu ya fedha ya namna ya kuweka akiba,
usimamizi wa fedha binafsi na namna ya kujipanga na maisha ya uzeeni,
alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo
Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini
Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa
Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Tehama Mwandamizi, Idara ya kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga
(kulia), akimwelekeza Mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Godfrey Msambwa, namna ya
kupakua Application ya GePG inayorahisisha kulipia malipo ya huduma za
Serikali, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya
Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane,
Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa
Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya
Fedha, Bw. Fronto Furaha (kulia), akiwaelezea wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Marie De Mathias ya jijini Dodoma, kuhusu majukumu ya Wizara hiyo katika
kusimamia Uchumi, wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika
Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya
Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi
Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Ramadhan Mbalamwezi (Kushoto) akiScan Msimbo
wa QR yenye maelezo kuhusu Mfumo wa Hazina ya Machapisho wa Wizara ya Fedha,
wakati alipotembelea Banda la wizara ya hiyo, katika Maonesho ya Kimataifa ya
Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini
Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa
Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Kulia ni Afisa Maktaba
Mwandamizi kutoka Wizara hiyo, Bw. Tumaini Katabazi.
Afisa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa
Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Amosi Ndegi (kulia), akitoa elimu kuhusu Mfumo wa
Taifa wa Ununuzi (NeST) kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma, waliotembelea
Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika
katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya
“Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Habari Mwandamizi, kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Farida Ramadhan
(kulia), akiwaelezea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Marie De Mathias ya jijini
Dodoma, kuhusu huduma zinazopatikana katika Banda la Wizara, wakati
walipotembelea katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika
katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya
“Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi”.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
No comments:
Post a Comment