PSSSF YATOA SH.MILIONI 10, KUSAIDIA MATIBABU YA WATOTO WENYE MARADHI YA MOYO - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 16 August 2024

PSSSF YATOA SH.MILIONI 10, KUSAIDIA MATIBABU YA WATOTO WENYE MARADHI YA MOYO

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Yesaya Mwakifulefule (kulia), akimkabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Mwakilishi wa CRDB Bank Foundation, Bi. Joycelean Makule, kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye maradhi ya moyo na akina mama wanaosumbuliwa na changamoto ya Fistula, kupitia mbio za CRDB  marathon. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar Es Salaam Agosti 16, 2024.

........................................

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetoa msaada wa shilingimilioni 10 kwa lengo la kuboresha huduma za afya nchini, kupitia mbio za CRDBMarathon.

Akikabidhi msaada huo Agosti 16, 2024 kwenye Makao Makuu ndogo ya PSSSF jijini Dar EsSalaam, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bw. Yesaya Mwakifulefule amesema,PSSSF imeungana na CRDB ili kusaidia juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya na hivyo kusambaza tabasamu kwa wenye uhitaji na jamii nchini, ambapo fedha zitakazopatikana zitakwenda kuwasaidia watoto wenye maradhi ya moyo na akina mama wanaougua Fisgtula.

“Sisi tunaamini, miongoni mwa watoto watakaotibiwa, miongoni mwa akina mamawatakaotibiwa wako wanachama wetu ambao kupitia mbio hizi tunakwenda kuwagusa.”Amefafanua Bw. Mwakifulefule na kjuongeza….Sisi peke yetu tungehitaji fedhanyingi kufanikisha suala hili, lakini tunapoungana pamoja, sisi PSSSF, CRDB na wadau wengine wanaounga mkono mbio hizi basi changamoto za watoto na akina mama hawa zinakwenda kutatuliwa.” amesisitiza.

Akitoa neno la shukrani, mwakilishi kutoka CRDB Bank Bi. Joycelean Makule,  ameishukuru PSSSF kwa msaada huo ambao amesema unakwenda kusaidia mipango muhimu ya afya ili kusaidia jamii ya Watanzania.

“Mbio hizi zimeanzishwa ili kuhakikisha watanzania wenyewe tunajenga utamaduni wa kuweza kutatua matatizo yanayotuzunguka, na hili tumeona ni jukwaa zuri kushirikiana na watanzania, na mwaka huu tumeweza kushirikiana na jumla ya watu 8000.” amesema.

Aidha, amesema mbio za CRDB Marathon zinatarajiwa kufanyika Agosti 18, 2024, jijini Dar Es Salaam. Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Yesaya Mwakifulefule (kulia), akimkabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10, Mwakilishi wa CRDB Bank Foundation, Bi.Joycelean Makule, kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye maradhi ya moyo na akina mama wanaosumbuliwa na changamoto ya Fistula, kupitia mbio za CRDB marathon. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar Es Salaam Agosti 16, 2024.

Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Yesaya Mwakifulefule, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwakilishi wa CRDB Bank Foundation, Bi. Joycelean Makule, akizungumza kwenye hafla hiyo.Baadhi ya watumishi wa PSSSF, watakaoshiriki mbio hizo wakionesha jezi watakazo zitumia siku hiyo. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages