GAVANA: WATEJA WATAREJESHEWA FEDHA ZAO KULINGANA NA KIWANGO CHA BIMA - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 8 August 2024

GAVANA: WATEJA WATAREJESHEWA FEDHA ZAO KULINGANA NA KIWANGO CHA BIMA

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

........................... 

Na John Buuku, Dodoma 

SERIKALI kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema itaendelea kusimamia Benki zote nchini kwa kuzingatia viwango vya Kimataifa, huku wakitoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha benki kutokana uendeshaji wa uchumi wa kisasa unategemea zaidi matuminzi ya utaratibu wa kibenki ambapo kwa sasa umerahisishwa.

Akizungumza leo Agosti 7, 2024 katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Emmanuel Tutuba, amesema kuwa ni muhimu kuhifadhi fedha benki kwani ni sehemu salama.

“Ukitunza fedha nyumbani kuna athari nyingi zinazoweza kujitokeza ikiwemo kuibiwa, kuungua moto, lakini ukitunza Benki na ikitokea changamoto yoyote unarejeshewa fedha zako” amesema Gavana Tutuba.

Gavana Tutuba amesema kuwa BoT kupitia Bodi ya Bima ya Amana (DIB) wameweka utaratibu mzuri wa kurejesha fedha za wateja kama ikitokea benki imefilisika.

“Benki ikifungwa serikali itahakikisha wateja wote waliojitokeza watarejeshewa fedha zao kulingana na kiwango cha bima pamoja na kuwafatilia wateja wote waliokopa ili waweze kurejesha madeni yao” amesema Gavana Tutuba.

Amesema kuwa DIB imeongeza kiasi cha kurudisha fedha kwa wateja kutoka milioni moja hadi milioni saba na Laki tano wakiwa na lengo la kulinda amana ya mteja. 

Gavana Tutuba amefafanua kuwa kwa mujibu wa tathmini waliofanya mwezi june mwaka huu inaonesha kuwa benki zote zina ukwasi pamoja na mitaji ya kutosha.

“Kiwango cha mikopo chechefu imeshuka hadi kufikia asilimia 4.3 ambacho ni kiwango kipo chini na ukilinganisha na utaratibu wa kimataifa” alisema Gavana Tutuba.

Katika hatua nyengine amewakumbusha watanzania ambao walikuwa wanahifadhi fedha benki ambapo kwa sasa benki hiyo imefilisika kwenda Ofisi ya DIB kwa ajili kuchukua fedha zao kama bado hawajachukua.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba akionesha furaha na viongozi mbalimbali waliotembelea banda la BoT.
Furaha ikitamalaki wakati wa maonesho hayo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages