BoT YALENGA MFUMUKO WA BEI KUBAKI KATIKA LENGO LA KATI - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 2 August 2024

BoT YALENGA MFUMUKO WA BEI KUBAKI KATIKA LENGO LA KATI

Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Marwa Patrick akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la BoT ili kupata elimu ya fedha kwenye banda la BoT katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma. 

................................

Na Mwndishi Wetu, Dodoma 

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imelenga mfumuko wa bei ubaki katika lengo la kati la asilimia tatu na tano. 

Hayo yamebainishwa Leo Agosti 2, 2024 na Marwa Patrick Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT   wakati alipokuwa akizungumza kwenye banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma. 

Amesema jukumu la BoT ni kuhakikisha kiwango cha fedha kwenye mzunguko kinakuwa kipo sawia na malengo mapana ya kiuchumi. 

“Mwaka huu tunamakadirio ya ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.4 ambapo mwaka jana uchumi ulikuwa kwa asilimia 5.1,sisi watu wa sera ya fedha tunajukumu la kuhakikisha fedha zilizoko kwenye mzunguko zinachangia kufikia haya malengo ya kuwa na mfumuko wa bei ambao uko wigo wa 3 na 5”, amesema. 

Ameeleza kuwa BoT inajukumu la kuhakikisha fedha zinakuwa sawa na endapo ikitokea zikawa nyingi na kushindwa kufikia malengo wanaziondoa na zikiwa chache wanaziongeza kwenye mzunguko kwakutumia nyenzo za sera ya fedha. 

“BoT inaweza kuyakopesha mabenki ya biashara fedha kwa muda maalumu, na tunapolazimika kuziondoa fedha zilizozidi inabidi tukope pia kuna njia nyingine ya kuziondoa fedha kwakuipandisha riba ya benki kuu mfano riba tuliyokuwanayo kuanzia Julai hadi Septemba ni asilimia sita na tukiona kuna vihatarishi mbalimbali vya mfumuko wa bei tunaipandisha hii riba ya benki kuu kutoka asilimia 6 hadi 7”, amesema. 

Amesema wanavyoipandisha riba wanafanya mazingira ya kifedha kuwa magumu na mabenki ya biashara yatakapo kuja kukopa kutakuwa na ugumu kutokana na riba hiyo kuwa juu hivyo kuifanya fedha kurudi katika kiwango cha kawaida. 

Aidha, amesema wanamajukumu mbalimbali katika utendaji wao wa kazi ikiwemo kutoa takwimu za kiuchumi,wanafanya tafti za masuala ya fedha na uchumi pamoja na kuandaa ripoti mbalimbali za kiuchumi.Meneja Mawasiliano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msina akimkabidhi zawadi mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 2, 2024.Meneja Mawasiliano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msina pamoja na Mariam Kopwe kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT wakiwa kwenye banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 2, 2024.


Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Marwa Patrick akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la BoT ili kupata elimu ya fedha kwenye banda la BoT katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma. Afisa wa Benki Kuu (BoT) kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki , Geofrey Jonas Valonge kushoto na Francis Mdoe Afisa wa Benki Idara ya Huduma za Kibenki BoT Dodoma wakiwaonesha noti halisi na noti bandia baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo. 


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages