.............................
Na Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za
hisani za Benki ya Maendelo zenye lengo ya kusaidia vituo viwili vya watoto kwenye
Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro ambapo itasaidia watoto waliozaliwa chini
ya miezi 9 pamoja na kituo cha watoto yatima cha Mtoni Dikonia kilichipo
Bagamoyo mkoani Pwani.
Mbio hizo zitafanyika tarehe 7.9.2024 kwenye Viwanja vya Farasi Jijini Dar es salaam hayo ameyasema Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Maendeleo, Emanuel Mwaya Jijini Dar es salaam Julai 24.2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema watoto wengi wamekuwa wakifariki wakikosa huduma mbalimbali ikiwemo vitanda na vifaa mbalimbali .
“Katika Hospitali ya KCM zaidi ya watoto 500 wanazaliwa kila mwaka lakini
uhitaji ni mkuwa kuliko vifaa vinavyohitajika na kwasababu hiyohiyo watoto
wengi wamekuwa wakifariki kwa sababu ya kukosa huduma mbalimbali ikiwemo
vitanda na changamoto nyingine.
“Takwimu zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 25% mpaka 30 ya watoto wanaofika pale watoto karibu 150 kati ya 500 wanafariki moja ya sababu kubwa iliyotajwa ni ukosefu wa vifaa”amesema Emanuel. Kauli mbiu ya mbio hizo ni hatua ya faraja msimu wa pili.
No comments:
Post a Comment