Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude (Katikati), akizungumza na
wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa
nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting)
unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho ,
ambapo washiriki zaidi ya 2,000 kutoka nchi za Afrika na unalenga kujenga Imani
ya umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika, Bi. Malehlohonolo
Mahase, na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha
(AICC), Bi. Christine Mwakatobe.
...................................................................
Na. Peter Haule na Joseph Mahumi, WF, Arusha
Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wahasibu
Barani Afrika (African Association of Accountants General Meeting (AAAG))
utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka 2024,
ukiwahusisha zaidi wa washiriki 2,000 kutoka takriban nchi 55 za Bara la
Afrika.
Hayo yameelezwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, wakati wa
mkutano na Waandishi wa Habari jijini Arusha, uliolenga kuujulisha umma kuhusu
mkutano huo na fursa za kiuchumi na kijamii kwa watanzania.
CPA Mkude alisema kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa
kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, hususan
kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.
Alizitaja faida nyingine za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuwa na Afrika
yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji jumuishi na maendeleo endelevu, Bara
jumuishi lililounganishwa kisiasa na kwa kuzingatia maadili ya Pan-Africanism.
Aliyataja manufaa mengine kuwa ni pamoja na kuwa na maono ya Mwamko wa
Afrika na Afrika yenye utawala bora, demokrasia, kuheshimu haki za binadamu na
utawala wa sheria, Afrika yenye amani na usalama na Afrika yenye utambulisho
thabiti wa kitamaduni, urithi wa pamoja na maadili.
CPA Mkude alisema kuwa Mkutano huo utawaleta Wahasibu wakuu wa Serikali
Afrika watakaoambatana na Wahasibu Wakuu wa Wizara, Taasisi za umma na Wahasibu
na wadau wengine ambao watapata fursa ya kusikiliza mada za masuala mbalimbali
ya kitaaluma na kubadirishana mawazo na kujua fursa zinazopatikana katika nchi
za Afrika.
Alisema wageni kutoka nje watakuja na fedha za kigeni ambazo watazitumia
hapa Tanzania kwa kuwa watatembezwa kwenye mbuga za Wanyama na vituo mbalimbali
vya utalii na hivyo kuunga mkono dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kuutangaza
Utalii wa Tanzania.
Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa nyumba za wageni (hoteli), usafiri,
mamalishe na jamii kwa ujumla kuchangamkia fursa hiyo ya ujio wa wageni ili
kunufaika kiuchumi na kijamii.
“Natoa wito kwa Maafisa Masuuli wa Wizara na Taasisi zote kuwaruhusu
Wahasibu, wakaguzi na wadau wengine watakaoomba kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Pili
wa Wahasibu wakuu wa Serikali Afrika, African Association of Accountants
General (AAAG) utakaofanyika jijini Arusha mwezi Desemba, 2024”, alisema CPA
Mkude
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni
Mhasibu Mkuu wa nchi ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase, alisema Mkutano wa
Wahasibu Afrika unafanyika Tanzania kwa kuwa ni mwanachama anayeaminika na
amekuwa mshiriki mwaminifu katika umoja huo, na kwamba wajumbe wa mkutano huo
wanakuja kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua kubwa katika matumizi ya
mifumo ya fedha.
Alisema kuwa Tanzania ipo vizuri katika kutekeleza viwango vya kimataifa
vya kihasibu, imekuwa ya mfano katika ukuaji wa Uchumi, imeimarika katika suala
la ukarimu wa wageni, maendeleo katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano na
ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi vya utalii hivyo wanachama kuna mambo
mengi ya kujifunza.
Aidha alieleza kuwa Mkutano huo utakao wakutanisha pia Jumuiya za
wafanyabiashara watapata fursa ya kujua ni namna gani Afrika ipo tayari katika
suala la uwekezaji na namna ya kuripoti hali ya Uchumi ya Afrika, jambo ambalo
litaongeza uwazi na uwajibikaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC),
Bi. Christine Mwakatobe alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wageni
wanapokuja wanapata huduma bora kwa kuwa wanaamini watakuwa mabalozi wa
Tanzania na watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii.
Alisema anamshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuitangaza nchi yetu Duniani
na kwamba hauo ni matunda ambayo Taasisi za Serikali kwa ujumla zinafaidi kwa
kazi yake anayoifanya, huku Kituo chake cha Mikutano kikihudumia mikutano mingi
ya Kitaifa na Kimataifa.Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude (Katikati), akizungumza na
wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa
nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting)
unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho ,
ambapo washiriki zaidi ya 2,000 kutoka nchi za Afrika na unalenga kujenga Imani
ya umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika, Bi. Malehlohonolo
Mahase, na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha
(AICC), Bi. Christine Mwakatobe.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, akizungumza na wanahabari
katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha
(AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi
za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting),
unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho
cha AICC, na utawashirikisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka nchi za Afrika na
mkutano huo unalenga kujenga Imani ya umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha
za Umma kwa Ukuaji Endelevu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika ambaye pia ni Mhasibu Mkuu
wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase, akizungumza wakati wa Mkutano
na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa
nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting)
unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo amesema kuwa Mkutano huo
utakawakutanisha pia Jumuiya za wafanyabiashara na watapa fursa ya kujua ni
namna gani Afrika ipo tayari katika suala la uwekezaji na namna ya kuripoti hali
ya Uchumi ya Afrika, jambo ambalo litaongeza uwazi na uwajibikaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Bi.
Christine Mwakatobe, akizungumza kuhusu fursa ambazo Tanzania na wakazi wa mkoa
wa Arusha watapata wakati wa Mkutano na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano
katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano
wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association
of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5
Disemba Mwaka huu, katika Kituo cha AICC, ambapo amesema kuwa wamejipanga
vizuri kuhakikisha wageni wanapokuja wanapata huduma bora na watakua mabalozi
wazuri wa Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny
Mwaipaja, akiongoza Mkutano wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo
cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa
Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of
Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba
Mwaka huu, katika Kituo hicho cha AICC, ambapo Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA
Leonard Mkude, Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu
Mkuu wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase na Mkurugenzi Mkuu wa
AICC, Bi. Christine Mwakatobe, wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo
unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza
sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii, hususan
vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha, Bw. Renatus Msangira
(Kulia) na Mhasibu Mkuu Msaidizi wa Serikali, Bw. Victus P. Tesha, wakifuatilia
Mkutano na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu
Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG
Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo
hicho cha AICC, ambapo Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, Mwenyekiti
wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya
Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase na Mkurugenzi Mkuu wa AICC, Bi. Christine
Mwakatobe, wamewaleza wanahabari kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa
makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania,
hususan kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko katika ukanda wa
Kaskazini.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude (Katikati), Mwenyekiti wa Umoja
wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa nchi ya Lesotho, Bi.
Malehlohonolo Mahase (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mikutano wa
Kitamaifa (AICC), Bi. Christine Mwakatobe, wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya Mkutano wao na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha
Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa
Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of
Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba
Mwaka huu, katika Kituo hicho, ambapo wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo
unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza
sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii hususan
vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude (kushoto) na Mkurugenzi
Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha, Bw. Renatus Msangira, wakiteta jambo
wakati wanawasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano
Arusha (AICC), kufanya Mkutano na wanahabari, kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa
Kimataifa wa Wahasibu Wakuu wa nchi za Afrika (African Association of
Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba
Mwaka huu, katika Kituo hicho, ambapo wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo
unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza
sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii hususan
vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)
No comments:
Post a Comment