Naibu Kamishna wa TIRA, Bi. Khadija Said, akifungua mafunzo ya siku ya moja Huduma za Bima Mtawanyo (BankAsuarance) kwa Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo vya Habari, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
...........................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), imeipongeza Benki ya NMB kwa
kukuza Uelewa, Ufahamu na Elimu ya Bima kwa Jamii, huku ikivitaka vyombo vya
habari nchini kuisaidia Serikali kuibeba kwa uzito mkubwa agenda hiyo ya
kimkakati kuipeleka kwa Watanzania.
Pongezi na wito huo umetolewa leo Alhamisi Julai 18 na Naibu Kamishna wa
TIRA, Bi. Khadija Said, alipokua akifungua mafunzo ya siku ya moja Huduma za
Bima Mtawanyo (BankAsuarance) kwa Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo
vya Habari, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Bi. Khadija alimwakilisha Kamishna wa TIRA kufungua mafunzo hayo
yaliyohusisha mada mbalimbali zikiwemo Bima ni Nini, Benki Wakala wa Bima, Kazi
za NMB Katika Uwakala, pamoja na Huduma za Kibenki na Bima Rafiki kwa
Wanahabari zilizotolewa na Meneja Mwandamizi wa Bima wa NMB, Martine Massawe.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Bi. Khadija alisema NMB imechukua hatua
kubwa kwa kutenga muda wa kutoa elimu kwa wahariri na wanahabari waandamizi,
ambao kwa kutumia vyombo vyao vya habari, wataongeza uelewa na elimu ya bima
kwa jamii, ambalo ndio lengo chanya la Serikali.
“Niwapongeze NMB kwa mchango mkubwa katika kukuza uelewa wa elimu ya bima
kwa jamii, inachofanya hapa ni kutekeleza Mpango Mkakati wa Serikali na Mpango
Mkakati wa TIRA, unaotaka kufikia mwaka 2030, asilimia 80 ya Watanzania wawe na
elimu ya bima na asilimia 50 kati ya hao wawe wanatumia Huduma za Bima.
Alibainisha ya kwamba Miongozo ya BenkiBima (BankAsuarance) imetolewa kwa
mujibu wa Sheria, Kifungu cha 6(2) na Kifungu cha 11(A na B) ya Sheria ya Bima
Sura ya 314, ambacho kinataka Mamlaka kuweka vigezo vya Bima vinavyopaswa
kuzingatiwa na Taasisi za Fedha katika utoaji bima.
Bi. Khadija alikiri ya kwamba Benki Bima ni sekta inayokua kwa kasi nchini,
ikihusisha Sekta ya Fedha na Sekta ya Bima yenyewe, siri ya ustawi na ukuaji
huo sio tu suhirikiano baina ya taasisi hizo, bali pia mchango mkubwa wa vyombo
vya habari katika kujenga na kuimarisha uelewa
No comments:
Post a Comment