MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema amezungumza na Benki ya NMB kwa
ajili ya kukopesha mabasi 100 ya mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), ili
kutatua kero ya uhaba wa mabasi.
Mchechu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Julai 15, 2024 alipozungumza na
wahariri na waandishi wa habari jijini hapa kuhusu maandalizi ya kikao kazi cha
wakuu wa taasisi na mashirika ya umma.
Kwa mujibu wa Mchechu, mabasi hayo yatakayofika ndani ya miezi sita kuanzia
sasa, yatatoa huduma katika njia kuu pekee, huku katika njia za mlisho
ikisubiriwa utaratibu mwingine.
“Kesho (Julai 16) nitakuwa na kikao na NMB (benki) kwa ajili ya ununuzi wa
mabasi 100 na hivyo tutatatua changamoto ya uchache wa mabasi,” amesema.
Hata hivyo, amesema kwa njia zilizopo kunahitajika kampuni zaidi ya mmoja
kwa ajili ya uwekezaji akipendekeza ziwe tatu au nne kwa awamu zote sita.
No comments:
Post a Comment