BENKI YA CRDB YASHIRIKI SIKU YA USHIRIKA DUNIANI - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 8 July 2024

BENKI YA CRDB YASHIRIKI SIKU YA USHIRIKA DUNIANI


 Na Mwandishi Wetu

Benki yetu ya CRDB imeshiriki maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani (SUD) duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Tabora katika Viwanja vya Ipuli.

Maadhimisho hayo yaliyoanza tarehe 29 Juni 2024 na kuhitimishwa leo tarehe 6 Julai, yalifunguliwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa David Silinde na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko.

Mkurugenzi wetu Mtendaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Abdulmajid Nsekela aliungana na wafanyakazi wa Benki yetu kutoka Makao Makuu wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara, Maregesi Shaaban, pamoja na wafanyakazi wa Kanda yetu ya Magharibi wakiongozwa na Meneja wa Kanda hiyo, Jumanne Wagana.

Tukiwa mdau mkubwa wa sekta ya ushirika nchini, Benki yetu ambayo pia ndio mdhamini mkuu ilitumia maadhimisho hayo kuonyesha fursa za uwezeshaji zinazotolewa kwa wateja wake waliopo kwenye mnyororo wa thamani katika sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda na usafirishaji.

#CRDBBank

#UlipoTupo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages