Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (pichani) alivyoongoza uzinduzi
wa kampuni ya CRDB Insurance (CIC) ambayo ni moja ya kampuni tanzu nne za Benki
ya CRDB ikiungana na CRDB Bank Burundi, na CRDB Bank DR Congo na CRDB Bank
Foundation.
Pia alisema tukiwa wadau wa sekta ya fedha nchini tunatambua kuwa sekta ya
bima imeendelea kukua kutokana jitihada kubwa zinazofanywa na serikali na wadau
pamoja na matumizi ya teknolojia katika kutoa huduma hizi. Hata hivyo, bado
kasi ya ukuaji wa sekta hii si kubwa ikilinganishwa na nchi zingine barani
Afrika. Zipo sababu nyingi zinazochangia jambo hili ikiwamo ufahamu mdogo
kuhusu umuhimu wa bima miongoni mwa wananchi pamoja na uhaba wa huduma za bima
zinazokidhi na kuendana na mahitaji ya soko.
Aliendelea kwa kueleza kuwa tukiwa kama Benki kiongozi nchini, tuliona tuna
jukumu la kuchangia katika ukuzaji wa sekta hii ya bima nchini. Na kwa sababu
hii tuliona tusiishie tu kuwa madalali wa bima au kuuza bima kupitia kitengo
chetu cha Bancassurance, bali kuanzisha kampuni ya bima ambayo itakwenda kutoa
mchango katika changamoto zinazoikabili sekta ya bima nchini.
Kwa kumalizia alisema kuwa kwa niaba ya Benki ya CRDB kama muwekezaji mkuu
katika kampuni hii, tunajivunia uwekezaji huu tukiamini kampuni hii itafata
nyayo za kampuni mama katika kutoa mchango kwa Watanzania mmoja mmoja pamoja na
nchi nzima kwa ujumla. Mbali na kuweka juhudi za kutoa elimu ya bima ili
wananchi wengi waweze kujumuishwa katika huduma hizi, tunaamni CRDB Insurance
Company itaendeleza ubunifu kwa kuja na bidhaa za bima zinazokidhi mahitaji ya
makundi mbalimbali ya Watanzania hususan wale ambao wameachwa nyuma katika
huduma zinazotolewa sasa.
No comments:
Post a Comment