..............................
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya TADB imeendelea kutoa mafunzo ya uelewa kwa Benki washirika Kanda
ya Magharibi
Baada ya mkoa wa Tabora sasa ni Kigoma ambapo jumla ya wataalamu 24 kutoka
benki na taasisi za fedha washirika wa TADB mkoani humo, wamepatiwa uelewa
kuhusu TADB na huduma zinazotolewa katika kuchagiza utoaji wa mikopo na mitaji
kwenye mnyororo wa thamani wa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Pamoja na elimu kuhusu Mfuko wa SCGS na majadiliano ya ushirikiano wa namna
bora ya kufikisha huduma za fedha ikiwemo mikopo na mitaji kwa wakulima nchini
wataalamu hao pia wamefahamu kuhusu;
✅ Mikopo kwa taasisi za fedha
(Wholesale Lending Facility)
✅ Ufadhili wa pamoja wa
miradi ya kilimo (Co-financing
arrangement)
Kupitia Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS) @tadbtz inashirikiana na jumla ya benki na taasisi za kifedha 18 katika kuchagiza mageuzi ya kilimo nchini kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara.
#TADB
#KilimoKinaBenkika
No comments:
Post a Comment