DC Naano ameishukuru Bank ya NMB kwa kutoa msaada wa madawati ambayo yana kwenda kuondoa changamoto ya wanafunzi hao kukosa madawati ya kukalia wakiwa shuleni.
Aidha amewataka walimu wakuu wote
wilayani Bunda na maafisa elimu ngazi ya kata kuhakikisha wanayakarabati
madawati yote yaliyoharibika ili kupunguza changamoto ya watoto kukaa chini.
Mhe Naano amesema kuwa katika wilaya hiyo kuna upungufu wa jumla ya madawati elfu 16 katika jumla ya shule 188.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bunda Stoo Flaviani Chacha ameishukuru bank hiyo kuwa mdau wa karibu wa maendeleo huku akiwaomba wasiishie Bigutu tu bali waangalie namna ya kusaidia kwenye shule zingine.
Naye Dotto Makota akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa alisema baada ya kupokea maombi walikubali kutokana na kwamba wao ni wadau wa maendeleo ambo wanasaidia si katika elimu tu bali pia katika sekta zingine ikiwemo afya na majanga mbalimbali yanapotokea
No comments:
Post a Comment