Kwa mwaka huu, hili ni Gawio kubwa zaidi kutolewa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka taasisi za kibiashara ambazo Serikali ina umiliki wa hisa chache.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea mfano wa hundi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi NMB - Dkt. Edwin Mhede pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Bi. Ruth Zaipuna katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia ameipongeza Benki ya NMB kwa matokeo mazuri ya kiutendaji yaliyopelekea kuongezeka kwa faida kwa taasisi na gawio kwa Serikali.
Wakati wa hafla hiyo, Rais Samia pia aliikabidhi tuzo Benki ya NMB kutambua mchango wao katika kutoa gawio kubwa kwa Serikali mwaka hadi mwaka.Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bi. Ruth Zaipuna alisema: “Kutokana na mazingira wezeshi na uimara wa sekta ya kibenki, NMB ni miongoni mwa mabenki yaliyokua sana. Gawio la jumla limeongezeka kutoka Shilingi bilioni 97 mwaka 2021, hadi kufikia bilioni 181 mwaka 2023. Gawio kwa Serikali limeongezeka kutoka Shilingi bilioni 30.8 mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi bilioni 57.4 mwaka 2023.”
“Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuwa sehemu ya mafanikio haya,” alimalizia Bi. Zaipuna.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment