BENKI YA NBC YAKUTANA NA WATEJA WAKE WAKUBWA ARUSHA KUIMARISHA MAHUSIANO - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 23 June 2024

BENKI YA NBC YAKUTANA NA WATEJA WAKE WAKUBWA ARUSHA KUIMARISHA MAHUSIANO

 BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imekutana na wateja wake wakubwa yaani makamppuni na taasisi mbali mbali (Corporates) wa jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kupitia timu yake ya Biashara na Uwekezaji (CIB) mwisho wa wiki hii jijini Arusha, Mkurugenzi wa wateja wakubwa, taasisi binafsi na za serikali kutoka NBC, James Meitaron alisema tukio hilo ni muendelezo wa matukio kama hayo mahususi kwa wateja wakubwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Dodoma, Mwanza na Arusha.“Tukiwa kama muhimuli muhimu wa utoaji wa huduma za kifedha nchini, NBC tunatambua umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na kukuza ushirikiano kati yetu na wateja wetu. Hii inasababishwa na mabadiliko yanayotokana na ubunifu na maendeleo ya kiteknolojia.’’

"Hivyo hatua hii ya kukutana na wateja wetu wakubwa inatoa fursa kwetu kuelezea maboresho makubwa tuliyofanya kwenye huduma zetu sambamba na kutambulisha huduma mpya zilizorahisishwa zaidi kidigitali na zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu hususani hawa wakubwa." Alisema.

Aidha, kupitia mpango huo benki hiyo imekuwa ikielezea mikakati yake mipana inayolenga kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wateja hao, kuwajengea mitandao ya kibiashara miongoni mwao sambamba na kuwasogezea huduma za kibenki karibu zaidi huku huduma ya NBC Connect ikitajwa kama suluhisho muhimu katika kuwasogezea huduma za kibenki wateja hao wakubwa yakiwemo mashirika na kampuni binafsi, pamoja na taasisi za serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages