BENKI YA MKOMBOZI YAKUZA MIKOPO KUTOKA SH. BILIONI 28.8 HADI SH.BILIONI 134.3 - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 30 June 2024

BENKI YA MKOMBOZI YAKUZA MIKOPO KUTOKA SH. BILIONI 28.8 HADI SH.BILIONI 134.3

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande (wa pili kutoka kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Respige Kimati (katikati), pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo.

.........................................

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Chande (wa pili kutoka kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Respige Kimati (katikati), pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya Biashara Mkombozi, Gasper Njuu, amesema kwa kipindi cha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo, malengo ya benki, ikiwamo utoaji kwa Mtanzania, yamefanikiwa. 

Imekuza kiwango cha utoaji mikopo kutoka Sh. bilioni 28.8 Desemba mwaka 2013 hadi kufikia Sh. bilioni 134.3 mwaka jana, ikiwa ni ongezeko la asilimia 36 kwa mwaka. 

Amesema benki hiyo imeweza kutoa huduma za kibenki hasa mikopo midogo, kwa watu binafsi wakiwamo vijana na wanawake, kwa kuwapatia mikopo ya kati pamoja na mikubwa kwa makampuni, taasisi za huduma na wafanyabiashara. 

Gasper aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati benki hiyo ikitangazwa rasmi kupandishwa daraja na kuorodheshwa kwenye benki ya biashara katika soko la hisa. 

“Safari yetu katika Soko la Hisa la Dar es Salaam  Daraja la Soko la Ujasiriamali, imekuwa yenye mafanikio makubwa. Tumeshuhudia ukuaji mkubwa wa faida, ongezeko la amana za wateja, ongezeko la mikopo iliyotolewa kwa Watanzania. 

“Hii ni benki ya watu wote bila kujali itikadi zao za siasa, rangi, kabila au dini, tangu kuanzishwa kwa benki miaka 15iliyopita, kulikofuatiwa na kuorodheshwa kwa Benki katika Soko la Hisa la Dar es Salaam miaka 10 iliyopita,” alisema Gasper. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages