NMB YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA TABORA - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 18 September 2025

NMB YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA TABORA









BENKI ya NMB imefanya kongamano maalum na wafanyabiashara wa mkoa wa Tabora, likilenga kujadili fursa za kifedha na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.

Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara wa NMB, Dickson Richard, akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, amesema benki imejipanga kuendelea kushirikiana kwa karibu na wafanyabiashara katika kuwawezesha kifedha na kukuza biashara zao.

Kongamano hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara wa Tabora, likiwa jukwaa la kuimarisha mahusiano na kuonesha nafasi ya benki katika kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages