.................................................
Na Mwandishi Wetu
BANK of Africa -Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wake 20 wa kwanza wa wiki kupitia kampeni ya huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali iitwayo “MIAMALA NI FURSA”, ambapo kila mmoja amepokea zawadi ya Sh50,000 kwa kutumia huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi kupata huduma za huduma za kifedha.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya kampeni hiyo
iliyozinduliwa Juni 4, 2025, Afisa Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Bank of
Africa-Tanzania, Bw Lameck Mushi, alisema kuwa mwezi mmoja tangu kuanza kwa
kampeni hiyo ya miezi mitatu, imepokelewa vyema na umma wa Watanzania.
Bw Mushi alieleza kuwa kampeni hiyo inalenga
kuhamasisha matumizi ya jukwaa la benki kupitia simu kwa kuwazawadia wateja wanaofanya
miamala ya kila siku. Juhudi hizi ni sehemu ya dhamira ya benki yao kuendeleza
matumizi ya huduma za benki kidigitali na kuendeleza ujumuishwaji wa kifedha
nchini Tanzania.
“Tunafurahia mwitikio mkubwa tulioupokea hadi
sasa. MIAMALA NI FURSA tayari imefanya huduma za kibenki kupitia simu kuwa za
kuvutia na muhimu katika maisha ya kila siku ya wateja wetu,” alisema Bw Mushi.
Akiendelea, alisema ukweli kwamba “Wateja
wanashinda zawadi za fedha kwa kufanya miamala ya kulipa bili au kutuma fedha
unaonyesha kuwa vitendo vidogo, lakini vya mara kwa mara vina mchango mkubwa.
Zaidi ya hapo, tumeongeza unafuu kwa wateja wetu kwa kupunguza ada za miamala
ya Bank-to-Wallet kwa zaidi ya asilimia 50."
Kila wiki, wateja watano watakaokamilisha
miamala mitatu ya Bank-to-Wallet (B2W) na muamala mmoja wa ziada (malipo ya
bili, ununuzi wa muda wa maongezi au umeme) kupitia B-Mobile watakuwa na nafasi
ya kushinda.
Mwisho wa kampeni hii, ambayo itaendelea hadi
Septemba 2025, mshindi mkuu atajinyakulia zawadi ya pesa taslimu Sh5 milioni.
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa RejaReja Asupya Nalingigwa, alisisitiza: “Lengo letu ni kufanya huduma
za kibenki ziweze kufikiwa kwa urahisi, ziwe na manufaa na ziwaguse wateja wetu
kwa ukaribu zaidi. Iwe uko mjini au kijijini, mradi una B-Mobile, unaweza
kushiriki na kushinda.”
Ili kuhakikisha ushirikishwaji wa wote, Bank
of Africa-Tanzania imehamasisha timu zake za matawi kote nchini kusaidia
kuwaunganisha wateja wapya na kutoa mafunzo ya kutumia huduma hizo za
kidigitali. Timu maalumu ya msaada wa kiufundi pia ipo tayari kusaidia kutatua
changamoto zozote za upatikanaji na kuhakikisha uzoefu mzuri kwa watumiaji
wote.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Nandi Mwiyombella, aliongeza: “Kampeni hii si kuhusu zawadi
pekee, bali ni kuhusu kuwapa nguvu wananchi. Kwa kuhamasisha matumizi ya huduma
za kidigitali kwa njia shirikishi na rahisi, tunawasaidia Watanzania wengi
zaidi kushiriki katika mfumo rasmi wa kifedha.”
Kwa zawadi zaidi za fedha na washindi wapya kutangazwa kila wiki, Bank of Africa -Tanzania inawaalika wateja wake wote kufanya miamala, kushinda, na kufurahia huduma za kibenki kwa urahisi kupitia simu zao.
Kuhusu BOA Bank (T) Limited
BOA-Tanzania ni benki ya biashara binafsi
inayotoa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa, wateja wa kati (SME) na wateja wa
rejareja nchini Tanzania. Ilianza shughuli zake Juni 2007 baada ya kununua
Eurafrican Bank iliyokuwa ikifanya kazi nchini tangu Septemba 1995.
Benki hii ni sehemu ya kundi la Benki ya
Afrika, ambalo lilianza shughuli zake mwaka 1982 nchini Mali.
Kundi hili linafanya kazi katika nchi 19 za
Afrika, ikiwa ni pamoja na Afrika Magharibi, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati,
pamoja na ofisi za uwakilishi Paris (Ufaransa), Hispania, London (Uingereza) na
China. Tangu mwaka 2010, Benki ya Afrika imekuwa chini ya umiliki mkubwa wa
BMCE Bank, benki ya tatu kwa ukubwa nchini Morocco, inayotoa huduma katika nchi
31 na mabara 4.
Kwa sasa, BOA-Tanzania ina matawi 17 ya
rejareja, yakiwemo 8 Dar es Salaam na 9 katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Zanzibar
na miji mingine mikubwa.
Mawasiliano ya Vyombo vya Habari
Tovuti: www.boatanzania.com
Beatrice E. Mirigo – Maendeleo ya Bidhaa &
Mawasiliano
Barua Pepe: beatrice.mirigo@boatanzania.co.tz
Simu: +255 699 000 260
No comments:
Post a Comment