MABORESHO MAKUBWA YA BANDARI YAPAISHA UCHUMI WA NCHI - UMOJA BANKING BLOG

Home Top Ad

MABENK

Post Top Ad

Thursday, 6 March 2025

demo-image

MABORESHO MAKUBWA YA BANDARI YAPAISHA UCHUMI WA NCHI

Untitled-2

bandari
Muonekano wa Jengo la Ghorofa la  Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

..........................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 

Hali ya utendaji wa bandari TPA imeboreka ambapo shehena ya masoko ya nchi jirani iliyohudumiwa kupitia Bandari ya DSM imeongezeka kwa wastani wa asilimia 8.5 kwa mwaka, kutoka tani milioni 7.8 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 9.2 Mwaka wa Fedha 2023/24.

 

Kwa upande wa mapato ya Bandari (TPA tariff) yameongezeka kutoka shilingi trilion 1.1 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi shilingi trilion 1.475 Mwaka wa Fedha 2023/24.

[9:29 PM, 3/3/2025] +255 687 110 880: Tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie Madarakani hali ya utendaji wa TPA imeboreka ambapo katika kipindi hiki jumla ya shehena iliyohudumiwa na TPA imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 15.23 kwa mwaka kutoka tani milioni 20.78 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 27.55 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

 

Jumla ya shehena iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM iliongezeka kwa wastani wa asilimia 13.38 kwa mwaka kutoka tani milioni 18.67 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 23.98 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

 

Aidha Jumla ya shehena ya Makasha (Containers) iliyohudumiwa imeongezeka kwa wastani wa asilimia 12.9 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) laki 8.2 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) milioni 1.1 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

 

Kwa Bandari ya Dar es salaam

Jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM imeongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) laki 8.16 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) laki 9.98 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

 

Hayo yanatokana na maboresho makubwa ya Bandari za Tanzania yaliyofanywa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *