Serikali imeipongeza Benki ya CRDB kwa kudhamini Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Quran yaliyofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
Pongezi hizo zimeetolewa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa aliyemwakilishwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza ziara ya kikazi mkoani Tanga. Hata hivyo, Rais Samia alipita uwanjani hapo na kutoa baraka zake kwa washiriki.
Mashindano hayo yanayohusisha vipengele viwili kikiwamo cha watoto wenye umri chini ya miaka 13 na vijana wenye zaidi ya miaka 13, huwakutanisha washiriki kutoka maeneo tofauti duniani jambo ambalo Waziri Mkuu Majaliwa amesema linasaidia kuitangaza Tanzania.
“Mashindano haya yanahamasisha usomaji wa Quran Takufu, yanatoa fursa ya kujenga maadili mema, umoja, upendo na mshikamano pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa. Kupitia mashindano haya tunaimarisha diplomasia na biashara ikiwamo sekta ya utalii,” amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza:
“Nawapongeza Benki ya CRDB kupitia dirisha lenu la Al Barakah kwani mmetoa mchango mkubwa wa kufanikisha mashindano haya. Nawapongeza sana kwani ninyi pamoja na makampuni mengine mmeiwezesha shughuli hii kubwa ya kuwalea watoto katika misingi ya dini.”
Mheshimiwa Majaliwa amesema mashindano haya yanayowakutanisha Waislamu kutoka kila pembe ya dunia kuja kukumbushana umuhimu wa kusoma na kuitunza Quran Tukufu yanaikumbusha jamii kujenga utamaduni wa kukisoma kitabu hicho na vijana wanaoshiriki ni baraka kubwa mbele za Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema wakati wote taasisi hii kubwa ya fedha nchini inajielekeza katika kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja wake ndio maana huwa inajitahidi kubuni bidhaa zinazoendana na mahitaji ya soko.
Amesema dini ni nyenzo muhimu ya kujenga jamii yenye maadili, kuhamasisha amani na utulivu katika nchi yetu jambo linalowezesha sekta binafsi kufanya biashara na kutekeleza mipango yake katika kila uwekezaji.
Post Top Ad
Monday, 24 February 2025

SERIKALI YAIPONGEZA BENKI YA CRDB KUDHAMINI MASHINDANO YA QURAN
Tags
# Crdb
Share This

About BLOG
Blog hii ni kwa ajili ya kuripoti habari za Benki, Biashara, Fedha, Uchumi, Uwekezaji na soko la hisa sanjari na kuandaa makala za kuelimisha jamii masuala mbalimbali yanayohusu fedha. Tunafanya kazi masaa 24.
Newer Article
TANZANIA YANG’ARA SEKTA YA FEDHA AFRIKA
Older Article
TANZANIA'S REAL ESTATE REVOLUTION: A NEW ERA OF TRANSPARENCY & GROWTH
Tags:
Crdb
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment