BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI KUWEZESHA WATEJA KUFURAHIA PUNGUZO LA BEI ZA BIDHAA MSIMU WA SIKUKUU - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 13 December 2024

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI KUWEZESHA WATEJA KUFURAHIA PUNGUZO LA BEI ZA BIDHAA MSIMU WA SIKUKUU

Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakionesha bidhaa zao ambazo zinapunguzo la bei wakati huu wa msimu wa sikukuu.

...............................

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam


BENKI ya NBC imezindua msimu wa pili wa kampeni yao  inayofahamika kama "Tabasamu Tukupe Mashavu,"ikilenga kutoa fursa kwa wateja wao kufurahia pamoja na wapendwa wao wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki katika Sikukuu za mwisho wa mwaka kupitia punguzo la bei kwenye manunuzi ya huduma mbalimbali.

Kupitia kampeni hiyo, Benki ya NBC inalenga kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu, vocha za manunuzi pamoja punguzo la bei kwa asilimia hadi 10 kwenye huduma mbalimbali za kijamii na manunuzi ya vifaa vya kielectorinic huku zawadi kubwa kwa mshindi wa jumla ikiwa ni safari ya kitalii ya siku nne visiwani Zanzibar kwa mshindi na mwenza wake au rafiki.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika makao makuu ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo kampuni washirika wa kampeni ambao ni kampuni ya PUMA Energies, ABC Emperio, GSM, Johari Rotana, Bravo Coco, Numero Uno na wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara, Elvis Ndunguru.

Mabango yakioneshwa wakati wa uzinduzi huo.
Mahojiano na wadau yakifanyika
Furaha ikitamalaki wakati wa uzinduzi huo.
Mahojiano yakiendelea.
Mahojiano na wadau mbalimbali kuhusu huduma za benki hiyo yakiendelea

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages