BENKI ya NMB imetoa mamilioni ya fedha na vifaa ikiwemo zana za kilimo, friji na TV huku ikisubiri mshindi atakayeibuka na Sh100 milioni.
Zawadi hizo zimetolewa kwa washindi kutoka mikoa mbali mbali nchini kupitia Shindano lake la Bonge la Mpango linalochezeshwa kupitia matawi yake nchi nzima.
Meneja Mauzo wa NMB Makao makuu Nehemia Simba, amesema Shindano hilo linaendelea kuwaibua washindi kwa masharti nafuu ambayo ni kufungua akaunti tu.
"Kinachofanyika ni mtu kufungua akaunti na kuweka pesa kwa kiwango kisichopungua shilingi laki moja ndipo mtu anaingia kwenye Shindano,"amesema Simba.
Meneja huyo amesema wateja wengi wananufaika kupitia mpango huo ambao hivi karibuni walitoa zawadi katika Morogoro.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Ibrahim Sikana amesema utaratibu wa Michezo ya Kubahatisha unaoendeshwa na benki ya NMB umekuwa wa mfano na akaomba taasisi zingine zijifunze kupitia kwao.
Sikana amesema washindi kwenye mashindano ya NMB wanapatikana kwa njia
halali kwani mazingira ya Shindano ni ya wazi.
No comments:
Post a Comment