MKULIMA UKIWA NA UZOEFU WA KILIMO, KITAMBULISHO CHA NIDA UNAPATA MKOPO BENKI YA TCB - UMOJA BANKING BLOG

Home Top Ad

MABENK

Post Top Ad

Tuesday, 10 September 2024

demo-image

MKULIMA UKIWA NA UZOEFU WA KILIMO, KITAMBULISHO CHA NIDA UNAPATA MKOPO BENKI YA TCB

Untitled-2

IMG_8578Afisa wa Tanzania Commercial Bank (TCB),  Ramadhani Kassim

..............................

Imeandaliwa na Dotto Mwaibale

(0754-362990)

 

AFISA wa Tanzania Commercial Bank (TCB),  Ramadhani Kassim amesema mkulima mwenye uzoefu kidogo wa kilimo akiwa na kitambulisho cha Taifa (NIDA) anaweza kukopeshwa fedha na benki hiyo.


Kassim ameyasema hayo kwenye banda la benki hiyo lililopo kwenye Maonesho ya saba (7) ya kitaifa ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi  yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) yanayoendelea Uwanja wa Bombadia mjini Singida.


“Benki yetu inahusika kuwasaidia wakulima kuwapatia mitaji na mikopo ili waweze kufanya shughuli zao za kilimo popote pale nchini.


Alisema benki hiyo inawasaidia wakulima kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu baada ya kujaza fomu maalumu huku akiwa na viambatanisho kama kitambulisho cha taifa, barua inayomtambulisha mtaa anaoishi kutoka ofisi ya Serikali ya mtaa husika.


Aidha Kassim alisema ili mkulima aweze kukopeshwa na benki hiyo sifa nyingine awe na uzoefu wa zao analolilima walau kwa misimu miwili ili waweze kumfanyia utafiti kubaini mkopo ambao anaweza kupewa kulingana na kilimo anacho kifanya.


Kassim alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wakulima kutembelea banda lao lililopo kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kupatiwa mkopo kwa wale ambao watakidhi vigezo. 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages

undefined

Contact Form

Name

Email *

Message *