Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo, akipokea maua alipokuwa akipokelewa kwenye mkutano wa kuzungumza na wafanyabiashara.
...................................
Imeandaliwa na Dotto Mwaibale
(0754-362990)
RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipomteua Dkt.
Selemani Jafo kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara
akubahatisha kwani alikuwa sahihi na
alikuwa na malengo ya nchi kuwa na mtu atakaye weza kulipeleka mbele Taifa
kwenye uchumi mkubwa kupitia sekta ya viwanda.
Dkt. Jafo
aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hasan kushika nafasi hiyo Julai 2, 2024
akitokea Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ambako alikuwa akihudumu kama
Waziri.
Niseme tu kwamba Dkt. Selemani Jafo ni kiongozi mchapa kazi ambaye moto wake wa utendaji kazi ni uleule kwani alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) watanzania tuliiona kazi yake na hata alipohamishiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano Mazingira)nako tuliona kazi zake.
Kutokana na
kujituma kwake na kuwiwa kuwatumikia watanzania kupitia wizara mbalimbali
ambazo amekuwa akihudumu kama Waziri ni sababu kubwa inayomfanya azidi
kuaminiwa na Rais.
Dkt. Jafo
tangu alipoteuliwa amekuwa akifanya ziara mbalimbali za kutembelea na kukagua
miradi, viwanda na kuzungumza na Wafanyabiashara,wananchi, watendaji na
viongozi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake lengo likiwa ni kujua changamoto
na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbali ya
kujua changamoto pia ni kupanga mikakati endelevu ya kuona namna gani sekta ya
viwanda itaendelea kusonga mbele na kuinua uchumi wa taifa.
Haya yote anayofanya Dkt. Jafo
ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia aliyompa baada ya kumuapisha ambapo
alimtaka asiwe
kiongozi wa kukaa tu ofisini bali atoke kwenda kwa wananchi kuzungumza nao
na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika zinazihusu wizara yake.
Rais
Samia alimuambia Jafo kuwa alipokuwa Ofisi ya Makamu wa Rais alifanya vizuri na
ameona ampeleke Wizara ya Viwanda ili aweze kumsaidia kutokana na pilika nyingi
zilizopo kupitia wafanyabiashara
Rais
Samia alimtaka Waziri Jafo kuanza kazi yake kwa kufanya ziara eneo la Kariakoo
ambalo zuri na la kibiashara ambalo ni muhimu na ndilo linalolifanya jiji la
Dar es salaam kuwa ni kitovu cha biashara kutokana na kufikiwa na mataifa
mbalimbali huku ikizingatiwa kuwa Serikali imeweka fedha nyingi kwa kujenga
Soko la Kariakoo ili biashara ziweze kufanyika saa 24.
Baada
ya kufanya ziara hiyo ya kwanza ya kutembelea soko hilo la kimataifa la
Kariakoo binafsi kila wakati namuona akiwa kwenye ziara za kikazi au kwenye mikutano lengo likiwa
kuitumikia nchi kwa moyo wa kizalendo na kutekeleza maagizo ya Rais Samia
aliyomtaka asikae ofisini bali akafanye kazi.
Tangu
Dkt. Jafo aaminiwe na Rais na kupewa nafasi hiyo kwa muda mfupi amefanya mengi
lakini hapa nitayaeleza machache na anayafanya hayo ili kwenda na kasi ya
maendeleo ya Rais Samia.
Moja ya mambo ambayo ameyafanya ni pale alipotoa maagizo
kwa Taasisizote zilizo chini ya wizara ya Viwanda kutumia bidhaa za ndani za
ujenzi na kupiga marufuku uagizwaji wa vifaa hivyo nje ya nchi.
Maagizo hayo aliyoyatoa Julai 19,2024 jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya
kukagua na kuona maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) huku akisisitiza kuwa ujenzi wowote utakao anza vifaa vinunuliwe
ndani ya nchini.
Jambo lingine
aliloonesha kuwa anania ya dhati ya kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya
viwanda alisema Wizara ya Viwanda kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na Mkoa wa Lindi itaendelea kutafuta
wawekezaji sahihi wenye nia ya kuanzisha viwanda vipya na kufufua vilivyosimama
ikiwamo vya kubangua korosho mkoani Lindi ili kukuza uchumi na kuongeza fursa
za ajira.
Licha ya kufanya ziara hizo pia
amekuwa akitoa ushauri wenye tija kwa wamiliki wa viwanda ambapo Septemba 11,
2024 alikishauri Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo kuongeza kasi ya uzalishaji wa
sukari ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa sukari hasa katika kipindi
cha mvua ambapo viwanda vingi husimamisha zoezi la uzalishaji kutokana na
athari za mvua.
Dkt. Jafo akiwa katika ziara hizo amekuwa akizipongeza taasisi zilizo chini ya wizara hiyo ambazo zinafanya vizuri ambapo Julai 17, 2024 aliipongeza Wakala wa Vipimo (WMA) kwa utendaji kazi mahiri na wenye weledi na kutoa wito kwa Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara hiyo kuiga mfano wake.
Dkt. Jafo alikiri kuridhishwa kwa kiwango kikubwa na utendaji kazi wa WMA kupitia ziara yake hiyo alipotembelea Kituo cha Uhakiki wa Vipimo kilichopo Misugusugu Mkoa wa Pwani na kujionea utendaji kazi wake.
Katika kuhakikisha viwanda vinajengwa katika mikoa yote Dkt. Jafo aliwaagiza wakuu wote wa mikoa nchini kuhakikisha wanatenga maeneo ya uwekezaji wa viwanda wakati serikali ikiendelea kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi kuja nchini kauli aliyoitoa alipokuwa katika ziara ya kikazi alipotembelea Kiwanda cha Balochistan Group of Industry Limited (BGI) kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Akionesha
jinsi sekta ya viwanda inavyo kuwa kutokana na mikakati iliyopo akizungumza Julai 10, 2024 kwenye Mkutano wa wazalishaji wa sukari wa
nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika
Zanzibar Dkt. Jafo alisema uzalishaji wa
sukari kwa Tanzania Bara umeongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi ya miaka iliyopita
na ili kukidhi mahitaji yaliyopo kupitia kampuni za sukari inatarajiwa
kuzalishwa tani 706,000 ifikapo Mwaka 2025/26.
Dkt. Jafo alisema mkakati uliopo ni viwanda viendelee kufanya vizuri kwenye uzalishaji sukari ili kukidhi mahitaji ambapo kwa mwaka 2023/24, mahitaji ya sukari Tanzania yalikuwa takriban tani 807,000 na kuwa kati ya hizo tani 552,000 ni kwa ajili ya matumizi ya ndani na tani 255,000 zilizobaki zimetengwa kwa matumizi ya viwandani.
Waziri wa Viwanda, Dkt. Sulemani Jafo akikagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA katika ziara yake mkoani Lindi.Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo, akiweka Jiwe la Msingi katika Kituo cha Afya Lionja kilichopo Wilaya ya Nachingwea pamoja na kukagua ujenzi unaoendelea ikiwa ni mwendelezo wa Ziara Maalum Mkoani Lindi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Bweni la Watoto Maalumu katika Shule ya Msingi Mpilipili wilayani Lindi wakati akihitimisha ziara ya siku sita mkoani humo.
Waziri Jafo akihutubia katika moja ya mikutano yake wakati wa ziara ya kikazi mkoani Lindi
Waziri Dkt. Jafo akipata maelekezo alipotembelea alipotembelea Kiwanda cha Balochistan Group of Industry Limited (BGI) kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo, akizungumza alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Viwango house wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) unaoendelea Jijini Dodoma mapema.
Waziri Jafo akikagua ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo,akiangalia mbolea inayozalishwa na Kiwanda ya cha Intracom kilichopo Nala jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya kiwanda hicho lulai 8,2024.
Waziri
wa viwanda na biashara Dkt. Selemani jafo (Mb) akipokea maelezo ya jinsi mtambo
wa kisasa wa kupakia sukari unavyofanya kazi pamoja na mchakato mzima wa
uzalishaji sukari unavyofanyika kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya
Bakhresa Group Bw Hussein Sufiani alipotembelea kiwanda hicho Septemba 11, 2024
Ziara ikiendelea.
No comments:
Post a Comment