Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, akimkabidhi zawadi Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa baada ya kutembelea ofisi za makao makuu ya benki hiyo,
.....................................
Na Mwandishi Wetu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna amekutana na kufanya
mazungumzo na Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo haya yamelenga kuendeleza ushirikiano kwa ustawi wa mnyororo wa
thamani wa Sekta ya Ujenzi, na Mhe. Waziri amepata wasaa wa kuishukuru benki ya
NMB kwa kuwa mshirika wa karibu kwa wadau wa sekta hiyo.
Picha ya pamoja na Waziri Bashungwa.
Mazungumzo na Waziri Bashungwa yakiendelea
Mazungumzo yakiendelea.
No comments:
Post a Comment