
Na Chedaiwe Msuya, WF, Mtwara
Serikali kupitia Wizara ya Fedha imehitimisha mafunzo ya elimu ya fedha
Mkoani Mtwara ikiwa ni juhudi za
kuimarisha uelewa wa masuala ya kifedha miongoni mwa wananchi.
Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini
pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji na Dhamana, wametoa mafunzo
hayo kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara ambayo yalihusisha washiriki kutoka sekta
mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, wavuvi, makundi maalum na vijana
kutoka katika Wilaya zote za Mkoa huo
kuanzia tarehe 22 Julai,2024 na
kuhitimishwa tarehe 30 Julai, 2024.
Katika kuhitimisha zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya
Masasi, Bi. Beatrice Mwinuka ameishukuru
Wizara ya Fedha kwa kuwapa wananchi wa Mtwara uelewa na ujuzi wa kusimamia
fedha zao kwa ufanisi, kujua mbinu bora za uwekezaji, na kujiepusha na madeni
yasiyokuwa na ulazima yanayosababishwa na ukosefu wa elimu ya fedha miongoni
mwa wananchi.
Mada zilizofundishwa zilijumuisha jinsi ya kupanga mipango na kuzingatia
bajeti, kuweka akiba na uwekezaji, maandalizi kabla ya kustafu na namna ya
kutumia mikopo kwa uangalifu. Pia, washiriki walijifunza kuhusu uwekezaji
katika soko la hisa na fursa za kibiashara zinazopatikana kupitia miradi ya
serikali na sekta binafsi.
Washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali na kushiriki mijadala
iliyoongozwa na wataalamu. Mjadala huo uliwezesha watu waliofikiwa kuelewa
changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika kusimamia fedha zao na
kutoa suluhisho kwa vitendo.
Wananchi wameishukuru Wizara ya Fedha pamoja na wataalamu kwa mafunzo
waliopatiwa hatua ambayo itafanya mabadiliko makubwa katika shughuli zao za
Uzalishaji na hatimae kubadili hali za maisha yao ya kiuchumi hususan kwa
wananchi wa Mkoa wa Mtwara.
Katika hitimisho, washiriki walipongezwa kwa kushiriki kikamilifu na
kuahidi kutumia maarifa waliyojifunza kuboresha hali zao za kifedha na kiuchumi
kwa ujumla.
Wizara ya Fedha imeahidi kuendelea kutoa mafunzo kama haya katika maeneo
mengine ya nchi ili kufikia wananchi wengi zaidi.
Mafunzo haya yameonyesha mafanikio makubwa na matarajio ni kwamba yatakuwa
na mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha maisha ya wakazi wa Mtwara.
Ni matarajio ya Wizara ya Fedha kuwa mafunzo haya yatakuwa chachu ya
maendeleo endelevu katika jamii na kubadilisha hali za maisha ya wakazi wa Mkoa
wa Mtwara ambao wamekuwa wakipata vipato vikubwa katika shughuli zao za
uzalishaji lakini kiuhalisia hali za maisha yao yameonekana kutopiga hatua kutokana
na kuwa na matumizi mabaya ya fedha kutokana na ukosefu wa elimu ya fedha
miongoni mwao.
aadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Mbuyuni mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.
aadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Mbuyuni mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.
aadhi ya wajasiriamali na makundi maalum wa Mbuyuni mkoani Mtwara wakipatiwa mafunzo ya elimu ya fedha na Wizara ya Fedha wakishirikiana na Taasisi za Fedha mkoani Mtwara.
Afisa Mkuu wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bi. Gladness Lema, akitoa elimu ya Fedha kwa wanavikundi, wajasiriamali na makundi maalum katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbuyuni mkoani Mtwara.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Masasi, Bw. Peter Mushi, akizungumza na wananchi wa Mbuyuni wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yanayotolewa na watalaamu wa Wizara ya Fedha katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbuyuni mkoani Mtwara.Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Bi. Beatrice Mwinuka, (wapili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, walipofika Ofisini kwake kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wa Mtwara.
No comments:
Post a Comment