........................
Na Dotto
Mwaibale, Singida
WAENDESHAJI
wa Mashirika yasio ya Kiserikali (NGOs) Mkoa wa Singida wameombwa kuacha tabia ya
kutembea na fedha nyingi wanapokuwa wakifanya shughuli zao kwani kufanya hivyo kunahatarisha
usalama wa fedha.
Ombi hilo
limetolewa na Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Singida Emmanuel Kishosha wakati
akizungumza katika jukwaa la mashirika yasio ya kiserikali (NGOS), Agosti 22,
2024 Mkoa wa Singida.
“ Ndugu
zangu niwaombe msitembee na fedha nyingi mnapokuwa kwenye shughuli zenu za
kikazi badala yake ziwekeni benki kwa ajili ya usalama kwani benki yetu ya NMB
inamatawi kila sehemu mkoani hapa,” alisema Kishosha.
Kishosha alisema mashirika hayo yanaweza kukopesheka na benki hiyo na kuwa wao wanakopesha kuanzia mtu mmoja.
“ Ukitaka kwenda haraka nenda mwenyewe lakini ukitaka kufika mbali nenda na wenzako,” alisema Kishosha.
Alisema benki hiyo ipo wazi wakati wote na kama mashirika hayo yatahitaji kupatiwa mafunzo yanayohusu masuala ya kifedha wapo tayari kwani inawataalamu wa kutosha.
No comments:
Post a Comment