................................
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu Kasimu Majaliwa amewataka wafanyabiashara kuhakikisha
wanazingatia sheria ya alama za bidhaa ya mwaka 1993, iliyofanyiwa marekebisho
inayokataza kuingiza, kuuza na kuhifadhi bidhaa bandia kwani adhabu yake ni
kifungo na faini,”
Akisoma maagizo manne katika hotuba ya Waziri Mkuu leo Julai 18 ukumbi wa
Milimani City jijini Dar es Salaam kwa wadau mbalimbali wa udhibiti bidhaa
bandia Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe aliyemuwakilisha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amesema wadau wanatakiwa kuzingatia sheria ya alama
na kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC), kudhibiti bidhaa bandia ili kukuza
biashara na uwekezaji nchini.
Katika hotuba hiyo ya ufunguzi wa kongamano la kilele cha udhibiti wa
bidhaa bandia pia mada mbalimbali za udhibiti wa bidhaa bandia zimejadiliwa.
Akitaja maagizo mengine, amewataka wamiliki wa nembo nchini kuhakikisha
wanafuatialia bidhaa zao na kuziwasilisha FCC pale wanapogundua wafanyabiashara
wanatumia bidhaa zao zilizobadilishwa uhalisia.
“Endeleeni kutoa elimu kwa walaji juu ya athari za bidhaa bandia, ambapo
Wakala wa Forodha kwa kushirikiana na FCC
hakikisheni bidhaa bandia haziingii kupitia bandari na sehemu za
mipakani,”amesema
Ameitaka FCC kushirikiana na Taasisi zingine kudhibiti bidhaa hizo
kuhakikisha wawekezaji wanakuwa na imani, katika ukanda wa Afrika Mashariki
(EAC) na ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri Mkuu Majaliwa amesema, udhibiti wa bidhaa bandia sio jambo la mtu
mmoja, hivyo washirikiane wote kuhakikisha wanadhibiti suala hilo ambapo kazi
hiyo ikifanyika vizuri na kwa mafanikio
zaidi itavutia wawekezaji.
Amesisitiza FCC kuongeza wigo wa mashirikiano na mashirika mbalimbali ya
kimataifa ya biashara na udhibiti wa bidhaa bandia kuelimisha wadau kuhusu
madhara ya bidhaa bandia.
Amesema wamiliki wa bidhaa washirikane na FCC katika kutoa elimu ya alama zao na kushirikiana na mabalozi kuwaelemisha wafanyabishara wa nchi zao juu ya athari za bidhaa bandia.
No comments:
Post a Comment