
.......................
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Teknolojia na Mawasiliano Vodacom
Tanzania Plc imezindua kampeni kabambe inayojulikana kama “Ni Balaaa” ikiwa na
lengo la kuwanufaisha wateja wake na jamii nzima kiujumla. Kampeni hii kubwa na
ya kitaifa inalenga kunufaisha watanzania wengi ambapo kutakuwa na washindi wa
kila siku, wiki, mwezi na washindi watano wa zawadi kuu huku wote wakiondoka na
zawadi kemkem ikiwemo fedha taslimu.“Kampeni ya Ni Balaaa inalenga kuwazawadia wateja wetu kila wanaponunua
kifurushi (bando) au kufanya miamala kupitia M-Pesa na pia kutoa nafasi kwa
washindi wa zawadi kuu, kupendekeza Shule za Msingi katika Jamii zao na Vodacom
Tanzania itafanya maboresho katika maktaba za shule hizo kama vile kuwapatia
vitabu, makabati ya kuhifadhia vitabu na samani za kusomea”, alisema Grace
Chambua, Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kutoka Vodacom Tanzania
wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Kariakoo-Gerezani, jijini Dar es
Salaam.
Kampeni hii yenye kaulimbiu ya ‘Kila Mtu ni Mshindi’ inaanza mwezi huu wa
Julai mpaka Oktoba mwaka huu huku ikiwa na washindi wa kila siku wa shilingi
100,000/-, washindi wa wiki wa shilingi 500,000/- huku wale wa mwezi wakiondoka
na shilingi milioni moja, na washindi watano wa zawadi kuu ambao kila mmoja
ataondoka na kibunda cha shilingi milioni 20.
Akielezea namna ya kushinda kupitia M-Pesa, Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa
M-Pesa kutoka kampuni hiyo, alisema, “kila muamala unaoufanya kupitia M-Pesa
katika kipindi cha kampeni unaongeza nafasi yako ya kushinda. Iwe unatuma pesa
kwa familia, unalipia bili au unatumia M-Pesa super App kwa miamala na malipo
ya kila siku.”

“M-Pesa inamrahishia kila mtu kufanya miamala, ikiwemo wafanyabiashara kama nyie mliotuzunguka hapa Kariakoo. Yaani popote pale ulipo kila unapotumia M-Pesa basi moja kwa moja unaingia kwenye droo na hivyo kujiongezea nafasi ya kuibuka mshindi. Sisi tunasema Pesa ni M-Pesa na msimu huu “Ni Balaaa”, anamalizia Mbeteni.
Kwa kumalizia Bi. Chambua aliongezea kuwa kampeni hii itawagusa pia wamiliki wa biashara ndogo na za kati ambapo kwa kujiunga na SME Combo Bundles kutoka Vodacom sio tu zitawarahisishia shughuli zao za kibiashara, lakini pia zinawapa nafasi ya kushinda zawadi muhimu kama vile zana za usimamizi wa hesabu (inventory management system) au kamera za CCTV kwa ulinzi zaidi wa maeneo yao ya biashara.
No comments:
Post a Comment