Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Ziara hiyo itaanza katika mikoa ya Mara na Arusha tarehe 15 Julai 2024,
ikiwaleta moja kwa moja watoto wahusika wa katuni maarufu barani Afrika na
vipindi vya burudani, ikiwa ni pamoja na watoto wenye ulemavu. Iliyoandaliwa
ili kuhamasisha kujifunza kupitia michezo, ziara hiyo inatoa mchanganyiko wa
kipekee wa elimu na burudani.
"Katika Ubongo, tumejizatiti kutoa maudhui ya kielimu yatakayowezesha
viongozi wa kizazi kijacho barani Afrika," alisema Iman Lipumba,
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Maendeleo. "Ziara ya Kujenga Akili ni
ushahidi wa kujitolea kwetu kufikia watoto katika kila pembe ya nchi ili
kuhakikisha wanapata rasilimali na mafanikio.
Basi lenye chapa ya Ubongo litasafiri katika mikoa hiyo, likibeba wahusika
wa katuni na waburudishaji kwa ajili ya kufanya maonesho katika shule na vituo
vya kijamii.
Vilevile waatashirikisha watoto katika michezo ya kielimu na mashindano
huku ziara hiyo ikilenga kujumuisha sherehe za Mwisho wa juma katika kila mkoa
ambapo watoto na walezi wao wataweza kushiriki katika shughuli mbalimbali.
Wakati wa sherehe hizi, watoto na walezi watapokea zana maalum
zitakazosaidia mchakato wa ujifunzaji.
"Tunafurahi sana kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation na Hope
and Healing International katika ziara hii ya kukuza akili. Ushirikiano huu
unathibitisha dhamira yetu ya pamoja ya kutoa uzoefu wa kielimu wa hali ya juu
kwa watoto na walezi nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment