SHIRIKA la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO) wameendelea kutoa elimu katika Maonesho ya Kimataifa ya Dar Es Salaam maarufu kama Sabasaba yaliyoanza rasmi Juni 28 na yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2024.
Maonesho hayo yanayokutanisha wafanyabishara na wajasiriamali kutoka kila pande ya dunia ,TIRDO imeshiriki kwa kuonesha teknolojia mbalimbali za kitaalamu na za kiubunifu.
Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa Masoko wa TIRDO Burhan Mdoe amesema kuwa katika Maonesho hayo wamekuja na bunifu pamoja na teknolojia mbalimbali ambazo zinasimamiwa na TIRDO lakini pia zile zilizobuniwa na watafiti wa TIRDO.
Aidha Mdoe amezitaja teknolojia hizo kuwa ni Matumizi bora ya nishati Viwandani na Majumbani (Energy Efficiency), Upimaji wa ubora wa bidhaa bila kuharibu (non destructive testing) –NDT, Nishati safi ya kupikia (Clean cooking Energy), Utaalam wa Maabara ya chakula na bioteknolojia (Food and Biotechnology ) Mfumo wa ukusanyaji taarifa za Viwanda na fursa za uwekezaji Tanzania (National Industrial Information Management System)-NIIMS.
Pamoja na hayo Mdoe ametaja teknolojia zingine kuwa ni pamoja na Maabara ya upimaji wa ubora wa bidhaa za ngozi na taaluma atamizi zilizo chini ya TIRDO. Teknolojia zote hizo zinalenga kutoa taarifa na utaalam mbalimbali kwa wananchi wa katika Maonesho hayo.
Mzee Peter Chuwa ni mmoja wa watembeleaji wa banda la TIRDO ambapo alifurahia kupata taarifa juu ya namna uzalishaji wa mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya mimea na vyakula (Biomas) , Mzee Chuwa ambaye pia ni mdau wa sekta ya nisahati salama alishukuru kuongezewa ujuzi ambao ameahidi kwenda kuanzisha uzalishaji na kuahidi kuwakaribisha wataalamu kutoka TIRDO kwa ajili ya kumuongezea utaalamu zaidi.
No comments:
Post a Comment