Serikali inazindua Sera mpya ya Taifa ya Biashara ya 2003 Toleo la 2023 yenye dhamira ya kuweka mfumo na mkakati madhubuti unaolenga kuboresha mazingira ya biashara, kuongeza ajira, Pato la Taifa, ukuaji wa kiuchumi na kuboresha ustawi wa wananchi.
Amesema Sera hiyo mpya toleo la 2023
imeoanisha Sera na kanuni za biashara na Sera zinazohusiana na masuala ya
kibiashara, kuondoka mgongano wa kisheria, mgawanyo wa majukunu ya kitaasisi,
kuimarisha miundombinu ya masoko na biashara, kupunguzwa muda na gharama za
ufanyaji biashara, kuwezesha biashara mtandao, biashara ya huduma, usimamizi wa
ushindani halali wa kibiashara na kumlinda mlaji.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda
na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo Julai 28, 2024 Dar es Salaam alipokuwa
akiongea na Waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Sera hiyo utakaofanyika
Julai 30, 2024 jijini Dar es Salaam.
Aidha amebainisha kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Sera hiyo
inayoongozwa na kauli mbiu isemayo.
"ushindani wa biashara katika kuchochea kasi ya mabadiliko ya kijamii
na kiuchumi yanayoongozwa na viwanda" anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko.
Vilevile amebainisha kuwa hafla hiyo ya uzimduzi inajumuisha wadau mbalimbali wapatao 300
kutoka Taasisi za umma, Taasisi Binafsi,
Mashirika ya Dini, Wabia wa Maendeleo, Mabalozi, Vyama vya Wafanyabiashara na
wenye Viwanda na Wafanyabiashara.
Naye Mkurugenzi mkazi wa kampuni ya Trade Mark Afrika Elibariki Shammy aliipongeza Tanzania kwa kufanya maboresho hayo na kusisitiza kuwa ni vema kila Nchi ya Afrika liige hatua hiyo ili biashara ziweze kufanyika kwa urahisi kwa kuwa bado Sera nyingi zinakinzana.
No comments:
Post a Comment