SERIKALI KUTOA MITUNGI YA GESI YA SH. BILIONI 10 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/ 2025 - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 23 July 2024

SERIKALI KUTOA MITUNGI YA GESI YA SH. BILIONI 10 KWA MWAKA WA FEDHA 2024/ 2025

Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika mwaka huu wa fedha itatoa mitungi ya gesi takriban 400,000 kwa wananchi yenye thamani ya Shilingi bilioni 10.

Akizungumza na wananchi wiilayani Mbinga leo Julai 23, 2024, Kapinga amesema lengo la serikali ni kuongeza matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia nchini  kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira na kuwaepusha wananchi na maradhi yanayotokana na matumizi ya nishati isiyo safi.

"Hadi sasa kupitia REA tumeshatoa mitungi ya ruzuku 83,500 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.5 na kazi inaendelea." amesema Kapinga.

Ameongeza kuwa, nia ya serikali ni kupunguza gharama za vifaa vya nishati safi ya kupikia ili wananchi wapate huduma kwa bei nafuu.

Amesisitiza kuwa, serikali inaendelea kufanya mazungumzo na wadau ili kuongeza Mawakala hadi ngazi ya  Vijiji ikiwemo kutoa ruzuku kwa mawakala hao kupitia miradi mbalimbali.

(hii ni kwa hisani ya gazeti la Nipashe)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages