RAIS DKT. MWINYI ALIPO TEMBELEA BANDA LA BENKI KUU MAONESHO YA SABASABA - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 14 July 2024

RAIS DKT. MWINYI ALIPO TEMBELEA BANDA LA BENKI KUU MAONESHO YA SABASABA

 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania  (BoT, Bw. Emmanuel Tutuba.(kushto) akizungumza mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, alipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam Julai 13, 2024 ambapo aliyafunga maonesho hayo.

.................................

 Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba.

Katika ziara hiyo, Dkt Mwinyi amepewa maelezo kuhusu elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu kazi za Benki Kuu ikiwemo sera za fedha, namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali, mifumo ya malipo ya taifa, na namna BoT inavyosimamia sekta ya fedha nchini.

Vilevile, Gavana Tutuba ameeleza kuhusu kazi za kitengo cha kupambana na utakasishaji fedha haramu na kazi zinazofanywa na Bodi ya Bima ya Amana.

Rais Dkt. Mwinyi amefunga rasmi maonesho hayo ambayo yalianza Juni 28 na kufikia tamati leo Julai 13, 2024.

 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania  (BoT, Bw. Emmanuel Tutuba.(kushto) akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi baada ya kutembelea banda la benki kuu.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages