Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi Kanda ya Magharibi.
...............................
Na Mwandishi Wetu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna, akiambatana na
viongozi wengine wa Benki, amefanya ziara ya kikazi katika Kanda ya Magharibi
ya Tanzania, ikijumuisha mikoa ya Kigoma, Katavi, Tabora, Simiyu, Shinyanga, na
Mwanza.
Katika ziara hiyo ya wiki moja iliyomalizika jana, Bi. Ruth Zaipuna
amekutana na wafanyakazi wa Benki ya NMB, wateja, na wadau mbalimbali, akilenga
kuimarisha uhusiano na kutoa mwongozo kuhusu utekelezaji wa mikakati ya Benki
katika maeneo hayo.
Pamoja na mambo mengine, Bi. Ruth Zaipuna amefanya vikao na viongozi wa
baadhi ya mikoa hiyo yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha
na kuchangia katika ukuaji wa kiuchumi.
Aidha, ziara hiyo pia ilitoa fursa ya kusikiliza maoni na mapendekezo
kutoka kwa wadau na kudhihirisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma
zinazokidhi mahitaji ya Watanzania katika ngazi zote.
Ziara hiyo ni muendelezo wa juhudi zetu katika kuhakikisha huduma bora za kifedha zinawafikia Watanzania katika kila kona ya nchi.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment