Mkuu wa Polisi Kata ya Chapwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anthony Sabasaba akitoa elimu kwa wafanyabiashara mjini Tunduma mkoani Songwe ya kuchukua tahadhari wanapofanya shughuli zao ili wasiweze kutapeliwa na watu wahalifu.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Songwe.
MKUU wa Polisi Kata ya Chapwa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anthony Sabasaba
amewapatia elimu wafanyabiashara wa huduma za kifedha katika Mtaa wa Msapania
Mjini Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani Songwe.
Mkaguzi Sabasaba akizungumza na wafanyabiashara hao amewataka kuwa
waangalifu na kuongeza umakini wakati wanapo wahudumia wateja wao ili kuepuka
utapeli kwa njia ya mtandao.
"Fuateni masharti ya leseni zenu ikiwa ni pamoja na kupeleka hela za
mauzo Benki mapema na muache tabia ya kwenda nazo nyumbani ili kuepuka
kufanyiwa uhalifu" alisema Mkaguzi Sabasaba.
Pia aliwataka wafanyabiashara hao kuweka walinzi waliopitia mafunzo ya Jkt
au Mgambo katika maeneo yao ya biashara
kwa usalama wa mali zao.
Elimu ikiendelea kutolewa.
No comments:
Post a Comment