PATA MKOPO WEZESHI KUTOKA CRDB KUPITIA PROGRAMU YA IMBEJU - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 23 June 2024

PATA MKOPO WEZESHI KUTOKA CRDB KUPITIA PROGRAMU YA IMBEJU

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa (kulia) akimkabidhi Jarida Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International, Bi Prudence Masako waliposaidi mkataba wa mashirikiano.

...................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


 BENKI ya CRDB imeendelea kujipambanua baada ya kusaini makubaliano ya kushirikiana na Shirika la Care International kuwawezesha wanawake kupata mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa biashara, usimamizi wa fedha na mitaji, pamoja na kuwapatia mitaji wezeshi ya kujikwamua kiuchumi kupitia program ya IMBEJU. 

Akizungumza kwenye hafla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema taasisi hiyo inafurahia kuingia mkataba wa ushirikiano na shirika la Care International kwani utakwenda kuwezesha programu ya IMBEJU kuwafikia wanawake wajasiriamali wengi zaidi nchini. 

Tully amesema lengo ya programu ya IMBEJU ni kuongeza ujumuishi wa kiuchumi nchini, hivyo ushirikiano na Care International utakwenda kusaidia kufikia lengp hilo kwani shirika hilo limekuwa likijihusisha na uwezeshaji wa vikundi vya kiuchumi kote nchini kwa takribani miongo mitatu. 

Aidha, aliishukuru Serikali kupitia Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Tume ya TEHAMA (ICTC) kwa ushirikiano ambao wanautoa kupitia programu biashara changa bunifu za vijana. Hivi karibuni Benki ya CRDB ili tangaza matokeo ya programu shindani ya vijana ambapo vijana 706 waliwasilisha maombi huku 106 wakichaguliwa kushiriki mafunzo kabla ya kupewa mitaji wezeshi. 

“Programu ya wanawake kupitia IMBEJU bado dirisha lipo wazi, na tumeendelea kuongeza nguvu kwa kushirikiana na Care International ili tuwafikie wengi zaidi. Nitoe rai kwa wanawake wanawake wajasiriamali kuchngamkia fursa hii ili kuboresha shughuli zao,” aliongezea Tully akitoa hamasa kwa wanawake. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International, Bi Prudence Masako amesema CRDB Bank Foundation ni mbia muhimu kwao kwani juhudi zao za kukabiliana na umasikini zitafanikiwa kutokana na uhakika wa fedha za uwezeshaji kupitia programu ya IMBEJU. 

Kunufaika na uwezeshaji kupitia programu ya IMBEJU wanawake wanatakiwa kuwa katika vikundi na kisha kuwasilishwa maombi kupitia tawi lolote la Benki ya CRDB nchini, au kupitia mfumo wa uwezeshaji wa vikundi wa Care International. 

Vikundi vitatakiwa kusaini makubaliano ya kushiriki programu ya IMBEJU, na kisha kupatiwa mafunzo na Shirika la Care International au maafisa uweshaji wa CRDB Bank Foundation. Mitaji wezeshi wa kati ya shilingi 200,000/= na 3,000,000/= inatolewa kwa mwanachama mmoja mmoja wa vikundi baada ya kuhitimu mafunzo. 

Program ya IMBEJU ilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Machi 12 mwaka huu na kufungua dirisha la ufadhili kwa biashara changa za vijana na wanawake wajasiriamali. Zaidi ya Shilingi 5 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha vijana na wanawake kupata mtaji wezeshi wa kuendesha biashara zao kupitia programu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages