..............................
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NBC imekabidhi msaada wa viti 49 kwa matumizi ya wanafunzi wa
Shule ya Msingi Buguruni Viziwi ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za
Benki ya NBC kuboresha mazingira ya kusoma kwa wanafunzi wa shule ya Buguruni.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo ikihusisha uongozi
wa shule hiyo pamoja na wanafunzi huku benki ya NBC ikiwakilishwa na maofisa
wetu wakiongozwa na Meneja Mahusiano ya Umma na Mawasiliano, Bi. Brendansia
Kileo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Brendansia alisema msaada huo ni sehemu ya
jitihada za Benki ya NBC kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau mbalimbali
hapa nchini katika kuboresha mazingira bora ya utoaji elimu.
“Ili wanafunzi hawa waweze kufaulu vizuri wanahitaji kusoma kwenye
mazingira mazuri yenye miundombinu muhimu ikiwemo viti. Kwa kuliona hilo Benki
ya NBC tumeona ni vyema tuitikie wito wa hitaji la wanafunzi hawa kwa kuwapatia
viti hivi 49 ikiwa ni sehemu tu mahitaji yao mengine mengi. Tunaamini kwamba
tutaendelea kushirikiana nao kwenye mahitaji mengine kadiri itakavyowezekana,’’
alisema Brendansia.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa Mtendaji wa
Chama Cha Kuhudumia Viziwi Tanzania, Bw. Yassin Mawe pamoja na kuishukuru Benki
ya NBC kwa msaada huo, alisema viti hivyo vitaisadia shule hiyo kukabiliana na
changamoto ya uhaba wa miundombinu ikiwemo viti, huku akitoa wito kwa wadau
mbalimbali kuendelea kujitokeza ili kuisaidia shule hiyo.
#NBCDaimaKaribuNawe
No comments:
Post a Comment