Na Dotto Mwaibale
BENKI ya Dunia na Benki ya CRDB zimedhamini hafla ya utoaji wa Tuzo kwa
walimu walioshinda shindano la pili la stadi za kufundisha somo la Kiingereza
kwa shule za msingi.
Benki hizo zimefanya udhamini huo kwa kutambua umuhimu wa walimu hao kwa
kile wanacho kifanya kwa watoto hao ambao wanakwenda kushika nafasi mbalimbali
za uongozi na kuwa walimu wa kesho.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ambaye alizungumzia umuhimu wa Walimu kujua
kufundisha kwa kutumia lugha ya kiingereza.
Miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo alikuwa ni Makamu Mwenyekiti
wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu,Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye ni
Mbunge wa Singida Mjini Musa Sima ambaye alitumia nafasi hiyo kuwapongeza
walimu hao kwa kushinda shindano hilo.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki
ya CRDB jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
No comments:
Post a Comment