


“Kutokana mikakati tuliyojiwekea, Benki yetu imekuwa kinara katika uwezeshaji wajasiriamali kwani hadi Mei 2024 tulikuwa tumetoa zaidi ya shilingi bilioni 995.346 kwa zaidi ya wajasiriamali 21,470 katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya kilimo, ujenzi na makazi, miundombinu, usafirishaji, afya, elimu, nishati, madini, biashara na viwanda, pamoja na uchumi wa buluu ili kuimarisha shughuli zao,” amesema Mwile.
Mwile amesema sekta ya ujasiriamali imekuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa
uchumi wa mataifa mengi duniani kwa kuchochea ubunifu na uanzishaji biashara
mpya ambazo huongeza ajira na kuimarisha kipato cha watu binafsi na jamii kwa
ujumla.
“Kwa kuanzisha biashara ndogo na za kati, wajasiriamali huchangia moja kwa moja kwenye ukuaji wa pato la Taifa na kuongeza mapato ya serikali kupitia kodi. Sekta hii pia ina mchango mkubwa katika kuboresha teknolojia na kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa na huduma, hivyo kufanya uchumi kuwa na ushindani zaidi kimataifa,” amesema Mwile.
Taarifa za Umoja wa Mataifa (UN) zinasema wajasiriamali ni injini muhimu ya
kufanikisha utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDG) kwani kundi hili
linachangia asilimia 90 ya biashara zote zilizopo duniani ambazo hutoa kati ya
asilimia 60 mpaka 70 ya ajira zenye staha na kuchangia zaidi ya nusu ya pato la
dunia. Tanzania kuna zaidi ya biashara ndogo za ujasiriamali milioni 3
zinazowapa uhakika wa kipato wamiliki wake.Ili kumkuza mjasiriamali kuanzia ngazi ya chini kabisa, Mwile amesema
Taasisi ya CRDB Bank Foundation ambayo ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB
inatekeleza programu ya Imbeju inayotoa elimu ya ujasiriamali na fedha kwa
wanawake na vijana pamoja na kuwapa mitaji wezeshi inayoanzia shilingi 100,000.
Hadi sasa tayari programu hiyo imewafikia wajasiriamali zaidi ya 400,000 na
kutoa mitaji wezeshi zaidi ya shilingi bilioni 10.
No comments:
Post a Comment