BENKI KUU YAENDESHA SEMINA YA KUWAJENGEA UELEWA WA MASUALA YA UCHUMI WANAHABARI WA MIKOA SABA - UMOJA BANKING BLOG

Breaking

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 14 June 2024

BENKI KUU YAENDESHA SEMINA YA KUWAJENGEA UELEWA WA MASUALA YA UCHUMI WANAHABARI WA MIKOA SABA

Meneja Idara ya Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Bi. Victoria Msina, (kushoto)) akizungumza wakati  wa ufunguzi wa semina  maalum kwa waandishi wa habari kutoka mikoa saba yenye lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya uchumi. Kulia ni Mwnyekiti wa Semina hiyo ambaye pia ni Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) Deogratias Nsokolo na katikati ni Meneja Idara ya Uendeshaji Tawi la BoT Dodoma, Bw. Nolasco Maluli ambaye alikuwa mgeni rasmi.

.....................

Na Nyamizi Moses, Dodoma

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) katika juhudi za kuimarisha uelewa wa waandishi wa habari kuhusu majukumu na masuala ya uchumi na fedha, imeandaa semina maalum kwa waandishi wa habari kutoka mikoa saba ya Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Morogoro, Iringa, na Njombe. 

Semina hiyo ya siku tatu inayowashirikisha waandishi wa habari 40 inalenga kuwajengea uwezo wa  kuripoti kwa usahihi  masuala ya uchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Meneja Idara ya Uendeshaji Tawi la BoT Dodoma, Bw. Nolasco Maluli, alibainisha kuwa utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari umekuwa ukifanyika kwa zaidi ya miaka 12, ambapo umesaidia waandishi kupata ufafanuzi wa kina wa masuala mbalimbali ya uchumi na fedha na kuwawezesha kutoa habari kwa ufasaha kwenye vyombo vya habari.

"Tumeshuhudia kuboreshwa kwa kazi zinazofanywa na waandishi wa habari, ikiwemo kututafuta pale wanapohitaji ufafanuzi wa kina wa masuala mbalimbali," alisema Bw. Maluli. Aliongeza kuwa kwa miaka ya hivi karibuni, Benki Kuu imekuwa ikisikika sana kwenye vyombo vya habari na kwa sehemu kubwa kwa usahihi.

Mada kuu katika semina hiyo ni kuhusu Majukumu ya Benki Kuu, Mfumo mpya wa Sera ya Fedha ya kutumia Riba ya Benki Kuu, utekelezaji wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha, uwekezaji katika Dhamana za Serikali, na alama za usalama katika fedha pamoja na utunzaji mzuri wa noti na sarafu. Mada hizo zinatarajiwa kutoa uelewa mpana kwa waandishi wa habari na kuwasaidia kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo vyao vya habari.

Awali, Meneja Idara ya Mawasiliano BoT, Bi. Victoria Msina, amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa kuwa sehemu muhimu sana kwa Benki Kuu kuweza kuwafikia wananchi kupitia taarifa mbalimbali wanazozitoa, zikiwemo habari, makala, mahojiano, na vipindi maalum vya masuala yanayohusu uchumi, biashara na fedha. "Tunafarijika sana kwa kuwa mmekuwa daraja muhimu kati ya Benki Kuu na wananchi," alisema.

Semina hiyo inatarajiwa kuleta matokeo chanya katika uboreshaji wa uandishi wa habari za uchumi na fedha nchini.

Meneja Idara ya Mawasiliano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Bi. Victoria Msina, akisisitiza jambo kwenye semina hiyo.

Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi, Tawi la Benki Kuu Dodoma, Bi. Angela Abayo  akitoa mada kwa msisitizo..

Meneja Idara ya Uendeshaji Tawi la BoT Dodoma, Bw. Nolasco Maluli, akishiriki semina hiyo baada ya kuifungua rasmi.

Semina hiyo ikiendelea.Picha ya pamoja katika semina hiyo

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Pages